GET /api/v0.1/hansard/entries/1165794/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1165794,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1165794/?format=api",
"text_counter": 200,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "ambayo sasa ndio eneo jipya la kuimarisha uchumi, pia inatupiga chenga. Tukiangalia, tuna ufuo wa bahari kutoka Vanga, nyumbani kwa Mhe. Boy, mpaka Kiunga, upande wa kaskazini katika eneo la Lamu. Utapata ya kwamba ijapokuwa tuna bahari hatuna usafiri wa bahari, kwa mfano kutoka Lamu kwenda mpaka Kwale. Kuna usafiri wa kutoka Shimoni kwenda mpaka kisiwa cha Pemba na Zanzibar. Lakini sisi katika Kenya hatuna usafiri wa kutoka Shimoni mpaka Mombasa ama Kilifi mpaka Mombasa ama Mombasa mpaka Lamu ili kuhakikisha kwamba wananchi wetu wanapata usafiri wa njia rahisi ambao uko salama. Safari ya Lamu inafanywa zaidi ya magari ambapo tumeona ya kwamba siku za karibuni kumekuwa na visa vingi vya majambazi kuvamia mabasi na kupiga watu risasi kiholela. Huu uchumi samawati ni eneo zuri ambalo sisi kama kaunti za Pwani tumeweza kusimamia kuhakikisha kwamba tunapata usafiri na bidhaa za bahari kwa urahisi, tunaweza pia kupata watalii kuja maeneo yetu mpaka maswala ya kawi kutokana na upepo wa bahari inaweza kupatikana kutokana na rasilimali hii ya bahari. Bi. Naibu Spika, sisi katika kaunti za Pwani tuna nafasi kubwa ya kuweza kutumia sheria hii itakapopitishwa kuhakikisha ya kwamba kaunti zetu zinafaidika na rasimimali ambazo ziko. Jambo lingine la kusikitisha ni kwamba kaunti zenyewe zinatoza ushuru bidhaa ambazo zinatoka kaunti moja kwenda kaunti nyingine. Kwa mfano, Mombasa inatumia zaidi mawe ya kujenga manyumba kutokana na mawe ya"
}