GET /api/v0.1/hansard/entries/1165796/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1165796,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1165796/?format=api",
    "text_counter": 202,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "ambayo yanatoka Kilifi. Kwa hivyo, jiwe lile likitolewa Kilifi, limetozwa kodi na likiingia Mombasa pia linatozwa kodi. Mpaka juzi mahakama ikasitisha kodi ambayo inalipishwa na kaunti ya Mombasa kwa bidhaa kama hizo. Tunaona kwamba bidhaa zetu zinakuwa ghali na mara nyingi tunadidimiza wananchi wetu katika maeneo yale. Kwa mfano, jiwe likitoka Kilifi likifika Mombasa, linalipishwa Kshs60 lakini jiwe likitumiwa Kilifi, halilipishwi zaidi ya Kshs40. Kwa hivyo, tunaona kwamba hizi kodi ambazo zinalipishwa katika kila kaunti kwa mfano rasilimali ama bidhaa ya samaki imetoka Lamu inakuja Mombasa; italipishwa ushuru Lamu, ilipishwe ushuru Kilifi na ilipishwe ushuru Mombasa. Maeneo matatu yanalipisha ushuru na yote hii inakuja kuwa mzigo kwa yule mwananchi ambaye anakaa kaunti ile ambaye ndiye atakuwa mtu wa mwisho kutumia bidhaa ile. Hizi regional economic blocks zitasaidia pakubwa kuwanisha kodi ambazo zinalipishwa katika kaunti zile. Ili kama kwa mfano Kilifi wamelipisha kodi, Mombasa"
}