GET /api/v0.1/hansard/entries/1165803/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1165803,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1165803/?format=api",
"text_counter": 209,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Kaunti zote zikiungana pamoja kama jumuiya ya kaunti, kwa mfano Mombasa itapata nafasi kubwa ya kujiimarisha kiuchumi. Miji mingi ambayo ina bandari inaimarika kwa sababu ya biashara ya bandari kwa mfano Rotterdam ilioko Uholanzi wameweza kuimarika kwa sababu ya biashara ya bandari katika eneo hilo. Lakini kwetu, biashara ya bandari iliondolewa ikapelekwa Naivasha dry port ili kuimarisha usafiri wa Standard Gauge Railway (SGR). Hii ilikua ni makosa makubwa kwa sababu ile comparative advantage ambayo bandari ya Mombasa ilikua nayo, kuweza kuleta wafanyibiashara kutoka maeneo yote na kuleta mali kutoka sehemu zote, imepungua sasa na utapata biashara zimefungwa hivyo kuathiri kodi ambayo Mombasa ilikua inapokea kutokana na wafanyi biashara walioko pale. Bi. Naibu Spika, nikimalizia, nilimsikia Sen. Farhiya akizungumzia maswali ya kanuni; yaani regulations. The Cabinet Secretary in consultation with the Council ofGovernors may make regulations giving effect to the provisions of this Act. Nafikiri hii ni standard provision ambayo inapatikana katika sheria nyingi zinazopitishwa. Mimi naunga mkono sheria hii na itasaidia pakubwa kuimarisha rasilimali zetu za kaunti. Hii sheria ikitumika kikamilifu, hatuna haja ya kungoja kupewa"
}