GET /api/v0.1/hansard/entries/1165813/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1165813,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1165813/?format=api",
    "text_counter": 219,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bi. Naibu Spika, mimi na Sen. Farhiya tuko katika Kamati ya Sheria ya Seneti. Hivi majuzi tulikua tunaangalia kanuni ambazo zimeletwa za irrigation. Sheria ya irrigation ilipitishwa kutoka mwaka wa 2016 au 2017, na hivi sasa ndio tunamaliza kupitisha regulations zao. Kwa hivyo, si makosa. Hata tukiweka kwa sheria kwamba lazima walete regulations kwa muda wa miezi sita, haitawezekana, kwa sababu, lazima wazingatie maswala ya public participation, kuzichambua zile regulations mpaka tuone ziko sawa na mambo ya mashauriano baina ya ofisi ya mkuu wa sheria na wizara yote inachukua muda kiasi ambapo haiwezekani kufanya hivyo kwa miezi sita. Lakini ni swala ambalo linaweza kuwekwa katika sheria hiyo. Bi. Naibu Spika, nilikua nazungumzia CBC ambapo tunajaribu kuwapa watoto wetu vipakatalishi na laptops pia. Hatuwezi kuwa tunawapeleka katika teknolojia halafu huku nyuma tunawaregesha kwenye analogue ya kusukuma wheelbarrow na kufanya mambo kienyeji. Kwa hivyo, njia peke yake ya kuhakikisha kwamba kaunti zetu zinasonga mbele ni --- Namaliza Bi. Naibu Spika."
}