GET /api/v0.1/hansard/entries/1165932/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1165932,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1165932/?format=api",
    "text_counter": 114,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Ninamuunga mkono na pia ninamshukuru Seneta wa Mombasa Kaunti kwa kuleta Kauli hii. Bandari hii ni ya zamani. Tunakumbuka Bandari hii ilikuwa inatuika kwa biashara ndogo ndogo. Sio kama ile Bandari kubwa ya upande ule wa KPA . Bandari hii ilikuwa ya wafanyikazi na wafanyi biashara ndogo ndogo. Sio zile biashara kubwa kubwa za meli ama meli zile kubwa za kiutalii. Bandari hii ilikuwa inasaidia. Serikali inatakiwa kuwa na nia ya kusaidia wafanyikazi wadogo. Hii Bandari imekuwa ikiwasaidia wafanyibiashara wengi kama vile wa kuleta nguo kwa bei nafuu kutoka Kismayo ama Middle East . Vyakula kama tende na vinginevyo pia vilikuwa vilikuwa vikiingilia hapo. Samaki kama papa, ng’onda na vipugu walitwaaliwa hapa. Biashara hiyo iliwezesha Mkenya kununua chakula kutoka kwa bandari ndogo. Hii Kauli ikiwasilishwa kwa Kamati husika, itakuwa vizuri Wanakamati waende wajionee na wafahamu kwa nini ile bandari ilifungwa na kufanya wafanyibiashara wadogo kukosa mapato. Asante, Bw. Spika."
}