GET /api/v0.1/hansard/entries/1166243/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1166243,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1166243/?format=api",
    "text_counter": 41,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika. Namshukuru na kumsifu mama Julia Andifu ambaye ni Mkenya aliyeleta ardhihali hapa Seneti. Kitu cha kwanza, kwa mama ama familia kumpoteza mtoto katika ile miezi tisa alafu dakika za mwisho inaonekana kwamba maisha ya mtoto hayawezi kuwa au daktari kufanya uamuzi wa yupi ataponyesha na ni yupi hawezi kupona, ni jambo la kusikitisha na huzuni ndani ya familia. Nina hakika mama Andifu alipoandika ardhihali hii, akilini mwake alikuwa anatafakari uchungu wa mama. Kule nyumbani tunasema, uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi. Ardhihali hii ni changamoto sana kwa hili Bunge letu. Hakuna aliyependa kufiwa na mwana ama kumpoteza mtoto wakati kila mtu anajua ni mgeni anakuja katika familia. Ni wakati mwafaka sisi kama Wakenya tuanze kutafakari na kufikiria. Sio lazima baada tu ya kuzaa mtoto aliye hai mama ataenda likizo, hata huyu mama aliyeteseka kubeba mtoto akiwa na matumaini na hatimaye kuambiwa matumaini yake yameangukia patupu anastahili likizo kwani ni jambo la kusikitisha. Kamati itakayohusika na ardhilhali hii inatakikana ifanye haraka iwezekanavyo kwa sababu ni muhimu na njia moja ya kupea afueni familia ambazo zitapatikana na janga kama hili la kumpoteza mtoto kabla hajazaliwa. Naunga mkono kwa dhati."
}