GET /api/v0.1/hansard/entries/1166249/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1166249,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1166249/?format=api",
    "text_counter": 47,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii ili nichangie malalamiko yaliyoletwa na Bi. Julia Difu, kuhusu akina mama ambao mimba zao zimeharibika. Malalamishi hayo yanazungumzia mambo mazito kabisa katika sheria yetu na pia Katiba. Kila Mkenya ana haki ya kupewa huduma za afya za hali ya juu. Mambo ya uzazi ni mojawapo ya vitu muhimu sana katika afya ya binadamu. Kwa hivyo, haki za kina mama wanaojifungua lazima zilindwe. Tumeona kwamba sheria inabagua akina mama wanaojifungua kuchelewa na pia wanaojifungua watoto wasio hai. Swala hili lazima liangaliwe kwa haraka kwa sababu Wakenya wengi, hususan akina mama, wanapoteza haki zao ilhali sheria iko wazi ya kuangalia swala kama hili. Wengi waliyotangulia kuzungumza walitaja mambo muhimu lakini katika Kifungu cha Pili, Bi. Difu amezungumzia sheria ya afya na kutaja vitu vyote ambavyo vinaguza akina mama hapa Kenya. Tumepiga hatua fulani katika nyanja za afya. Kwa mfano, Wizara ya Afya imeleta mpango wa “Linda Mama”. Hata hivyo, mara nyingi huu mpango unawalinda akina mama waliozaa watoto walio hai. Mpango huo hauwatunzi wale ambao wamejifungua kuchelewa. Bw. Spika, ipo haja kuhakikisha sheria hii ichunguzwe haraka ili kusuluhisha malalamiko ya Bi. Difu."
}