GET /api/v0.1/hansard/entries/1166367/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1166367,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1166367/?format=api",
    "text_counter": 165,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika wa Muda kunipa fursa ya kuchangia Mswada huu kuhusu elimu ya watoto wenye mahitaji maalum. Kwanza kabisa nawapa kongole Sen. (Dr.) Musuruve na Sen. (Prof.) Kamar kwa kuleta Mswada huu katika Bunge la Seneti. Maseneta hawa wawili wana tajriba katika mambo ya elimu. Kwa hivyo, Mswada huu ambao wameuleta ni wa muhimu sana kuhusu elimu ya wanafunzi wenye mahitaji maalum. Desemba mwaka jana, Siku ya Watu Wanaoishi na Ulemavu, nilibahitika kutembelea shule ya watoto wenye akili thaathira mjini Mombasa, yani Mombasa School for the Mentally Handicapped. Nilipofika pale, watoto wote walikuwa na furaha kwa sababu walikuwa wameelezwa kuwa kuna mgeni angewatembelea. Tulikula chakula cha mchana na wao kisha tukacheza mpira kidogo. Hata hivyo, niliona kwamba ipo haja ya shule kama hizo kupewa kipaumbele na misaada maalum ili kuhakikisha kwamba watoto walioko pale wanaangaliwa na wanapata chakula na mahitaji yao yote kisawasawa. Nilisikitika kwamba tangu shule hiyo kujengwa zaidi ya miaka 10 iliyopita, haijafanyiwa ukarabati wa aina yoyote na watoto walioko pale wote ni wenye akili thaathira. Wasaidizi pamoja na walimu wa watoto hao wanafanya kazi kubwa sana. Wengi wetu tutukipata watoto wenye akili thaathira, mara nyingi hatutaki watoke nje kwa sababu ni aibu. Unyanyapaa ama stigma inatokana na watu kutokubali kwamba mtoto kama huyo ni kiumbe cha Mwenyezi Mungu kama wengine, na kwamba akipelekwa kwa taasisi, itasaidia pakubwa kuboresha maisha yake na kumfanya mtu wa kutegemewa katika siku za usoni. Bwana Spika wa Muda, tukija katika Mswada huu, niko na mambo mawili ambayo ningependa kuzingatia. Kwanza kabisa ni kuwa, ingekuwa kuna kipengele cha kusema kwamba elimu hii ya watoto ambao wanamahitaji maalum ifanywe ya kwamba ni elimu ya bure. Wanafaa wasiwalipishe watoto wakiingia katika taasisi kama zile kwa sababu hivi sasa, wengi wanataka watoto wao wakasome. Lakini, wengi pia ni maskini na hali ya uchumi imewabana kiasi ambacho hawawezi kupeleka watoto katika shule hizi kwa masomo ikikumbukwa kwamba wale walimu ambao wanaosomesha katika shule hizi sio walimu wa kawaida. Ni walimu ambao wamefundishwa au wamefanyiwa mafunzo ya taaluma yao kwa njia ya juu. Kwa hivyo wanahitajika kulipwa pesa zaidi kuliko wale walimu wa kawaida. Bwana Spika wa Muda, naona ya kwamba kungekuwa na kipengee kwamba watoto wanaopelekwa katika shule zenye mahitaji maalum wawe hawalipishwi karo yoyote katika shule zile na kwamba ni jukumu la Serikali kuhakikisha tahasisi zile zinapewa fedha za kutosha. Nimeona hapa kuwa kuna swala la facilitation, lakini facilitation ni kitu ambacho hakiko wazi. Walimu wanaweza kupewa facilitation au wanafunzi wapewe vifaa vya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}