GET /api/v0.1/hansard/entries/1166368/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1166368,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1166368/?format=api",
"text_counter": 166,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "kusoma, vitabu na venginevyo lakini swala muhimu ni kwamba kuwe na fedha za kutosha ambazo zinapelekwa katika tahasisi hizi kuhakikisha kuwa wale watoto wanaosoma pale wanapata elimu ya hali ya juu na mazingira yao yako sawa kuweza kuishi katika eneo lile. Ningependa pia kujiunga na wale wenzangu walikuwa wametangulia kusema kwamba Mswada huu ni mzuri sana kwa masomo ya watoto wenye mahitaji maalum. Kwa hivyo, ni jukumu letu kuona kuwa Mswada huu umepitishwa ili wale watoto ambao wanazaliwa na mahitaji maalum kwa mfano, viziwi, vipofu, bubu, wale ambao akili zao zina tahadhira waweze kupata elimu ambayo itawasaidia maishani mwao na siku za mbeleni. Bwana Spika wa Muda, naunga mkono Mswada huu na nitakomea hapo. Asante."
}