GET /api/v0.1/hansard/entries/1167322/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1167322,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1167322/?format=api",
"text_counter": 46,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kieni, JP",
"speaker_title": "Hon. Kanini Kega",
"speaker": {
"id": 1813,
"legal_name": "James Mathenge Kanini Kega",
"slug": "james-mathenge-kanini-kega"
},
"content": " Asante sana Mheshimiwa Spika. Kwa heshima ya Mhe. Kamoti ambaye wakati mwingi alipenda sana kuongea Kiswahili, nataka kumpea mkono wa buriani. Kwa familia yake, ningependa tutoe bega la kujiegemeza wakati huu mgumu wakati wamempoteza mmoja wao. Tulichaguliwa pamoja na marehemu Mhe. Kamoti. Tumekuwa na yeye na nilimjua vizuri. Nimeshawahi elekea mpaka kwao Pwani kwenye Eneo Bunge la Rabai. Alikuwa mpole sana lakini alipokuwa kule mashinani watu walimpenda sana. Tulipoenda na “Baba” miezi miwili iliyopita, tulikuwa na mkutano mkubwa wa kufana na alionekana mtu wa watu sana. Kwa niaba yangu, familia yangu na ninaowaakilisha Eneo Bunge la Kieni, ninatoa mkono wa buriani kwa familia ya mwenda zake, na tuiombee familia yake amani ili wawe na ujasiri wakati huu mgumu."
}