GET /api/v0.1/hansard/entries/1167327/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1167327,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1167327/?format=api",
"text_counter": 51,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, WDM-K",
"speaker_title": "Hon. Mbogo Ali",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": " Asante Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii kama Mbunge wa Kisauni. Kwa niaba ya watu wa Kisauni, ninataka kuchukua fursa hii kutoa pole zangu na kupeana mkono wa buriani kwa mwenzetu aliyetuacha jana kutokana na ajali ya barabarani. Mhe. Kamoti hakuwa Mjumbe tu bali aliishi eneo bunge langu. Eneo Bunge za Kisauni na Rabai zimeshikana. Kwa hivyo, ni mtu aliyekuwa karibu sana na mimi kwa sababu mahitaji yake kama mwananchi anayeishi katika eneo langu, yalinipitia ili niweze kuyatatua. Hivi majuzi, niliweza kutengeza barabara iliyopitia pale alipoishi marehemu Mhe. Kamoti, lakini Mwenyezi Mungu alikuwa na mipango mengine. Tumekuwa naye juzi alipokuwa anapeleka makaratasi yake pale Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC), akawa cleared na akapewa cheti chake. Ni wakati alipokuwa akirudi nyumbani, ndipo maafa yakampata barabarani. Nachukua fursa hii kwa niaba yangu na kwa niaba ya watu wa Kisauni, kutoa pole nyingi sana kwa familia ya marehemu Kamoti. Asante, Mhe. Spika."
}