GET /api/v0.1/hansard/entries/1167420/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1167420,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1167420/?format=api",
    "text_counter": 144,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "kupewa nguvu ili iweze kuangalia zile pesa kwa makini na kina, ili ifanye kazi ya Wabunge ya uangalizi. Inasikitisha kuwa kuna maeneo yaliyotengwa kupewa fedha sawa na maeneo yaliyoendelea. Sababu ilikuwa kuwainua kimaendeleo wawe sawa na yale maeneo bunge yaliyo mbele kimaendeleo, kama barabara na vinginevyo. Inasikitisha kuwa kuna sehemu ambazo mpaka sasa bado zinajiita “jamii zilizotengwa”, ilhali pesa zinazopeanwa ni nyingi na inafaa ziwainue ziwalete hapo. Tutatengwa siku ngapi na tumepewa pesa na hatufikii wenzetu walipo? Hii itatusaidia sana. Kwa mfano, pesa ya NG-CDF zinasomesha kupitia kwa ufadhili. Katika Eneo Bunge la Lamu Mashariki, fedha za ufadhili ni zaidi ya milioni arubaini, ilhali wanafunzi sio wengi. Tunafaa tuwe na waliohitimu kama madaktari na watu wanaosimamia nyanja mbalimbali ili tuwafikie pale wenzetu walipo. Mpaka sasa, sisi tunalia tu kuwa tumetengwa, licha ya kupewa nafasi. Hii Kamati ikitilia mkazo, itasadia sana maeneo yaliyotengwa. Kitu kingine ambacho kinatusumbua na ambacho kitakachotufanya tuzidi kuwa nyuma na kujiita kutengwa ni wakaguzi. Wakifika Mjini Lamu, kwa mfano, watasema hapo ni maeneo ya"
}