GET /api/v0.1/hansard/entries/1167606/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1167606,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1167606/?format=api",
"text_counter": 330,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taveta, JP",
"speaker_title": "Hon. (Dr.) Naomi Shaban",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Mhe. Naibu Spika wa Muda, asante sana kwa kunipatia fursa hii. Hata mimi naunga mkono kuwa malipo ya wanakandarasi pamoja na wafanyabiashara wanaofanya biashara zao na kupatiwa kandarasi kupitia vitengo mbalimbali vya Serikali walipwe kwa wakati unaofaa. Kwenye kandarasi yoyote, kuna siku mtu ametarajia kulipwa. Wengi wa wafanyabiashara hao huchukua deni kupitia benki zao. Kunavyocheleweshwa, ndivyo wanavyoumia. Vilevile, wanakandarasi wengine kama wa ujenzi huchukua wafanyikazi kufanya vibarua ili wajimudu kimaisha. Huyu mwanakandarasi asipolipwa, wale vibarua pia huteseka. Faida kuwa mwanakandarasi alipata kazi ndiyo imfaidishe yeye na Wakenya wengine inakuwa ni shida. Bila kutatizika, ingewezekana Wakenya wanaopewa kandarasi walipwe kwa muda unaofaa. Hapa Kenya tungekuwa na wafanyabiashara na wanakandarasi ambao wamejimudu na kuwezesha wengine kujimudu kimaisha. Sheria hii itasaidia. Vilevile, ningependa kutaja kuwa wakati nilikuwa waziri katika Baraza la Mawaziri la Mhe. Rais Kibaki—ambaye ni mwendazake na Mwenyezi Mungu, amweke pahali pema peponi—alitoa mwelekeo kwa Serikali yake kuwa watu wasipeane kazi kama pesa hazipo kwenye wizara. Vilevile, maanake siko katika Baraza la Mawaziri, ingekuwa hivyo. Hilo lingewezekana tusingekuwa na madeni yanayongojea kwa miaka mingi bila kulipwa. Watu watakuwa wamefanya kazi wakati pesa tayari zimefika kwa wizara ama idara ambazo zinastahili kuwa na pesa zile na kupeana kandarasi. Naunga mkono. Sheria hii ikipita, itawezesha wanakandarasi kulipwa kwa wakati unaofaa. Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}