GET /api/v0.1/hansard/entries/1167773/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1167773,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1167773/?format=api",
"text_counter": 148,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Bw. Spika, nafikiri Kiongozi wa Wachache anataka kusema kuwa nimeshazungumza. Ni kama hataki niseme jambo lolote. Ukweli kuhusu mkopo ambao utachukuliwa wa zaidi ya Kshs1.1 billion ni kuwa watu wa Laikipia wamesema kwamba wakati huu hawawezi kujihimidi. Jambo lingine ni kuwa Kamati ya Fedha na Bajeti ya Seneti haikuniuliza kama vile tumekuwa tukifanya shughuli zetu katika Bunge hii. Ikiwa kuna Hoja ambayo inahusisha kaunti fulani, Seneta mwakilishi huitwa ili asaidie kuchanganua mambo. Bw. Spika, watu wa Laikipia wamesema kinagaubaga kuwa kukopa si kubaya, lakini hawataki mkopo wakati huu kwa sababu hawakuhusishwa. Kwa Kiingereza tunasema, public participation . Wamekubali kuwa kuna shida nyingi Laikipia ambazo zinahitaji fedha. Swali ni kuwa; fedha zilizotolewa na Serikali Kuu zaidi ya Kshs5.2 billion zimetumika vipi ndio tuwe wa kwanza kukopa? Kwa hivyo, nasimama hapa kupinga Hoja hii. Nitaipinga leo, kesho na hata milele, kwa sababu sheria haikufuatwa na watu wa Laikipia hawakuhusishwa kikamilifu. Naomba Maseneta wenzangu kupinga Hoja hii wakati tutakapopiga kura kwa sababu watu wa Laikipia wana shida nyingi. Pesa zikikopwa wakati huu, itakuwa vigumu kwao kulipa kwa sababu ya shida wanazopitia sasa."
}