GET /api/v0.1/hansard/entries/1167780/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1167780,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1167780/?format=api",
    "text_counter": 155,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Bw. Spika, Sen. Farhiya anasema ukweli kwamba kuna ushuru unaotozwa Laikipia. Hata hivyo, utozaji wa ushuru umekuwa ukikandamiza watu wa Laikipia kwa kuwa hawapumui. Ni kama jamaa wa kule Marekani kwa jina George Floyd alivyowekewa goti. Tunapowaambia hatupumui, bado goti linawekwa. Ijapokuwa kuna utozaji wa ushuru, ushuru huo umetukandamiza zaidi. Sasa wanataka kuchukua mkopo. Nataka kukuhakikishia kwamba hiyo itawafanya watu wa Lakipikia si tu kushindwa kupua bali pia kuaga dunia."
}