GET /api/v0.1/hansard/entries/1169097/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1169097,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1169097/?format=api",
    "text_counter": 88,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Seneta",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 611,
        "legal_name": "Mary Yiane Senata",
        "slug": "mary-yiane-senata"
    },
    "content": "Bi. Naibu Spika, ni ajabu kwamba bado Kamati inayohusika na mambo ya mafuta haijakaa chini tangu asubuhi mpaka saa hii kuyazungumzia hayo maneno yanayohusu bei ya mafuta. Tunajua kwamba bei ya mafuta inapopandishwa, itakuwa imepandisha pia bei ya vyakula, gharama ya kufanya ukulima, gharama ya kusafirisha vyombo vingine vyote ama bei ya kufanya biashara yoyote ile itakuwa imepanda. Gharama ya maisha pia itaendelea kupanda juu. Tayari, Wakenya walikuwa katika hali ngumu sana ya kimaisha. Wakenya wamekuwa wakisononeka hata kuweza kupata chakula mara mbili kwa siku imekuwa ngumu. Bei ya chakula ya kusafiri na ya ukulima inapokuwa juu, mwananchi wa kawaida kupata hata karo ya kulipia mtoto wa shule inakuwa ngumu sana. Bi. Naibu Spika, hii Statement ilitakiwa kupelekwa kwenye kamati leo na kamati hiyo ilifaa kukaa kesho kwa haraka sana kuweza kuongea na Wizara ya Nishati na Mafuta ili waweze kuhakikisha kwamba wamepata suluhu ya jambo hili. Tusiposuluhisha hili jambo la bei ya mafuta, inaonekana kila Mkenya atawacha gari lake nyumbani. Wakenya hawataweza kufika kazini kwa sababu hawataweza kumudu gharama ya tikiti ama ya kusafirisha bidhaa zao kupeleka kwa soko. Ningependa kuomba wanakamati wa Kamati ya Kawi waweze kukaa haraka kuzungumzia hili jambo la bei ya mafuta. Wakenya wanahofia ya kwamba itakuwa hali ngumu sana hasa tunapoelekea uchaguzi. Nimeskia ndugu yangu Sen. Olekina akisema"
}