GET /api/v0.1/hansard/entries/1169109/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1169109,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1169109/?format=api",
"text_counter": 100,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "ya Sen. Olekina imegonga ndipo kwa sababu kwa muda wa karibu mwaka mmoja, tumeona bei ya mafuta ikiendelea kupanda. Kwanza tuliambiwa ya kwamba hii shida imesababishwa na vita ambavyo vipo kati ya Russia na Ukraine. Lakini tumeona ya kwamba vita vinaendelea kwa muda wa miezi minne na hakujakuwa na upungufu wowote wa mafuta haya ambayo yanaongezwa bei mara kwa mara hapa nchini kwetu. Tutakumbuka ya kwamba bei za mafuta ilianza kupanda wakati kiwanda cha Kenya Petroleum Refineries kilipofungwa katika Mji wa Mombasa. Bi. Naibu wa Spika, hili ndilo jambo ambalo lilipelekea wengi kuagiza mafuta kibinafsi. Hiyo ndiyo inayosabisha mkurupuko wa bei ya mafuta kwa sababu hapakuwa na usimamizi wowote wa bei ya mafuta. Lazima Bunge la Seneti lishughulikie hili swala ambalo Sen. Olekina amezungumzia. Mimi ninaahidi ya kwamba iwapo Wataleta kanuni zao katika hili Bunge la Seneti, tutazichunguza kwa makini na kuhakikisha kwamba tumeondoa vipengele vyote ambavyo vitaendelea kudhuru Mkenya, kwa kuuziwa mafuta kwa bei ghali. Mafuta yakipanda bei, kila kila kitu kinapanda bei. Sio gharama ya kusafiri, bei ya vyakula na hata gharama ya kufanya biashara. Mafuta ni kitu muhimu. Ilisemekana kwamba tuko na mafuta katika Kaunti Turkana lakini tungekuwa tumeyaona. Meli moja peke yake ya mafuta ndiyo ilichukuliwa kuenda kusafishwa nje ya inchi. Mpaka leo, hatujaelezwa ilikuwa aje kuhusiana na hayo mafuta. Swala hili lazima liangaliwe kabla Bunge kuhairishwa kwa sababu ni jambo ambalo linaathiri Wakenya. Sisi ndio tunatarajia kuchaguliwa na Wakenya tarehe tisa Agosti, mwaka huu."
}