GET /api/v0.1/hansard/entries/1169115/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1169115,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1169115/?format=api",
"text_counter": 106,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Tunaona kuna uzembe fulani unaoendelea katika Wizaya Kawi. Wale wanaohusika, wakati mwingine wanaongeza bei vile wanavyotaka. Hali hii inafanya maisha ya Wakenya kuwa magumu sana. Tunaelewa kabisa ya kwamba unapoguza mafuta, umeguza maisha ya mwananchi. Utakuwa umeguza bei ya hospitali wagonjwa wanapoenda kutibiwa na bei ya chakula kupanda juu. Vilevile, haiwezekani kufanya maendeleo pasipo matingatinga kuenda katika mashamba. Bunge huwa halivunjwi; linahairishwa. Tuko na Kamati ambayo inahusika ya mambo ya kawi. Hili swala linapasa kupelekwa katika hiyo Kamati yetu ya Kawi, kuangaliwa na kuhusika katika hii kazi. Ninampa kongole tena ndugu yangu kwa sababu yeye huwa anaongea mambo ya Wamaasai sana. Leo ameongea habari ya bei ya mafuta. Wamaasai wote ambao kato Kaunti ya Narok, wakae wakijua ya kwamba Sen. Olekina ameweka rekodi kwa hii Nyumba, kwa kuleta Miswada ambayo inasaidia Wamaasai na pia Wakenya kwa jumla."
}