GET /api/v0.1/hansard/entries/1169269/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1169269,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1169269/?format=api",
    "text_counter": 260,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Kwanza, ningependa kuipongeza Kamati hii kwa kazi kubwa ambayo wamefanya kwa muda waliokuwa nao. Mimi nilibahatika kuhudumu katika Kamati hii kutoka mwaka wa 2018 mpaka 2020. Katika kipindi hicho, tulifanya kazi kubwa sana kwa sababu zile ripoti zote za mkaguzi kabla ya mwaka wa 2017, zilikuwa hazijachunguzwa bado. Kamati yetu ilihudumu na ikachunguza hizo ripoti zote na tukazileta katika Bunge hili la Seneti. Tuliidhinisha nyingi ya ripoti hizo lakini jambo la kusikitisha ni kwamba mpaka leo, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na taasisi za Serikali. Ninazungumzia taasisi"
}