GET /api/v0.1/hansard/entries/1169273/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1169273,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1169273/?format=api",
    "text_counter": 264,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": ". Madeni ya kaunti zetu yanaongezeka licha ya kwamba kulikuwapo na kamati maalum, ambazo ziliundwa na Council of Governors (CoG) pamoja na watu wengine. Walifanya uchunguzi wa madeni haya lakini mpaka leo, madeni yanaendelea kuongezeka. Haya yote yanatokana na unyonge ambao uko katika mabunge ya kaunti. Tumeona kwamba baadhi ya fedha hazichunguzwi na Seneti. Kwa mfano, fedha ambazo kaunti inakusanya yaani o wn source revenue, h aziangaliwi wala matumizi yake kuchunguzwa na Seneti. Inatakikana utumizi wa fedha hizi uchunguzwe na bunge la kaunti. Kuna unyonge mkubwa katika mabunge haya, hivi kwamba hawawezi kuchunguza hesabu hizo. Hata wakichunguza, wanafanya hivyo kwa uoga. Mwishowe, dhambi nyingi zinatendeka na fedha hizi pasipo kuchunguzwa bunge la kaunti au Seneti."
}