GET /api/v0.1/hansard/entries/1169274/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1169274,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1169274/?format=api",
    "text_counter": 265,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, pia tumeona ya kwamba ofisi ya Auditor-General mara nyingi wanakwenda vitandani na serikali za kaunti. Katika repoti zao unapata mambo ya kuwa mambo yale mazito; mambo yale makubwa ya ubadirifu wa pesa hawayaangazi, bali wanaangazia mambo madogo madogo kama vile kukosa kufanya bankreconciliation, kukosa kufanya cash and bank balances kwa usawa. Hayo ni mambo madogo madogo ambayo hayaonyeshi ubadhirifu wa pesa lakini zile fedha nyingi ambazo zinaliwa katika miradi ambayo haikamiliki zote huwa zinazibwa na ofisi ya Auditor-General na hivyo inakuwa vugumu kwa Bunge la Senate kuweza kuziangalia kama fedha hizo zimetumika kisawasawa. Jambo la nne ni kwamba, kwa sasa tunaelekea mwisho wa muhula wa magavana na muhula wa bunge, ipo hatari kwamba zile projects ambazo zimeanzishwa na magavana walioko ofisini sasa hazitaweza kukamilishwa na wale magavana ambao watachukua nafasi zile baada ya uchaguzi. Ipo haja ya Bunge hili kutoa mwongozo hususan kwa wakati huu kwamba miradi yote ambayo imeanzishwa lazima ipewe muda maalum wa kukamilishwa. Hiyo itapunguza ubadirifu wa pesa na vilevile itasaidia wanainchi kupata huduma kwa haraka iwezekanavyo. Jambo la mwisho ni kuwa, kaunti nyingi zimeshindwa kuongeza maradufu pesa ambazo wanakusanya katika maeneo yao. Kabla ya kuja kwa serikali za kaunti/ugatizi, kulikuwa na mabaraza ya miji na mabaraza ya wilaya ambayo ilikuwa inatumika katika"
}