GET /api/v0.1/hansard/entries/1169276/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1169276,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1169276/?format=api",
"text_counter": 267,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "kutoa huduma kwa wananchi katika sehemu zile. Mabaraza hayo yalikuwa yanakusanya fedha nyingi kiasi ambacho kiliweza kulipa mishahara, kutoa huduma na vilevile kupanga miradi ya maendeleo katika maeneo yao. Tukiangalia sasa, kaunti nyingi zinategemea pesa zinazotoka kwa Serikali kuu. Hii inazidi kutia unyonge kwa sababu pesa zikichelewa unasikia mishahara haijalipwa, watu hawaji kazi; unaskia mradi umekwama, watu wanagoma. Na hivyo basi, inatatiza huduma. Kama leo, kuna mambo mawili yamezungumziwa hapabunge kuhusiana na Garissa Teaching and Referral Hospital ambapo huduma zimedorora. Mhe. Sen, Ndwiga ameguzia kwamba katika Kaunti ya Embu pia huduma za afya zimedorora. Yote imesababishwa na kuwa pesa ambazo zinakusanywa katika maeneo yale hazikusanywi kisawasawa hakujakuwa na automation yaani ukusanyaji wa fedha unakwenda katika njia moja ya mfumo wa kitaalam wa kisasa ambao utahakikiska ya kwamba hakuna pesa ambazozinapotea Lazima maswala haya ya own source revenue yaangaziwe katika Seneti ijayo kwa sababu hiyo ndiyo njia pekee yake ya kuweza kuboresha huduma na kuboresha maendeleo katika maeneo ya kaunti hizi. Kama sivyo, itakuwa tunategemea Serikali kuu na Serikali yenyewe imebainika na kwa sasa hawatumii pesa kulingana na vile tunapitisha hapa kwenye CashDisbursement Schedule ambayo huwa inapitishwa na Bunge la Seneti ili kupeleka pesa katika kaunti hizi. Maswali haya lazima yaangaziwe katika Seneti Ijayo na zile repoti ambazo zimeletwa na zikapitishwa katika Bunge hili lazima zifanyiwe kazi ama sivyo, Bunge lijalo, jambo la kwanza ni kuwaita Directors wa DCI na EACC waje wajieleze ni sababu gani hizi ripoti ambazo zinatoka katika Bunge la Seneti hazifanyiwi kazi ili kuhakikisha ya kwamaba wale ambao wanafanya ubadhirifu wa pesa za umma wanapelekwa mahakamani na wanahukumiwa kulingana na sheria. Bi. Spika wa Muda, asante kwa kunipa fursa hii."
}