GET /api/v0.1/hansard/entries/1169304/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1169304,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1169304/?format=api",
    "text_counter": 295,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Ahsante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Mswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Watoto ambao umewasilishwa Bungeni na Kiongozi wa Wengi katika Bunge hili la Seneti. Kwanza kabisa, ningependa kusema kuwa Mswada huu unatilia nguvu Kipengele cha 53 cha Katiba ya Kenya kinachozungumzia haki za watoto. Ni Mswada unaolenga kutia nguvu haki za watuto, majukumu ya wazazi katika malezi ya watoto na njia mbadala za kulea watoto, uhifadhi wa watoto, kulinda watoto na jinsi ya kushughulikia watoto ambao wamekiuka sheria. Kwa sasa, mtoto akifanya makosa, polisi humweka pamoja na watu wazima. Hiyo inahujumu haki za watoto hao kisheria. Sheria hii inalenga kutoa mwongozo wa usimamizi wa huduma za watoto. Kutakua na baraza la kitaifa la huduma za watoto, yani the National Children ServicesCouncil, ambalo litaangazia maswala ya watoto. Mswada huu pia unalenga kulinda haki zilizotolewa kikatiba na mustakabali wa nchi hii kwa sababu watoto ndio watakaokuwa viongozi na kufanya kazi ili kujenga nchi yetu ya Kenya. Kwa hivyo, unalenga kulinda mustakabali wa nchi hii kwa ajili ya siku za usoni. Vile vile, Mswada huu unanuia kuzuia uharibifu wa maisha ya watoto kutokana na uhalifu ama matumizi ya dawa za kulevya na mambo mengine ambayo yanaathiri maisha ya watoto. Iwapo watoto wataachiliwa kuingilia dawa za lulevya na mambo mengine, hiyo itadhuru ustawi wa nchi hii kwa sababu hatutakuwa na vijana wa kutegemea siku za usoni ili kuendesha nchi hii. Mswada huu pia utalinda mustakabali wa watoto na wazazi wao. Kwa sasa, kuna visa vya wazazi kutojali maisha ya watoto wao. Wanakandamiza haki za watoto kwa njia moja au nyingine. Kwa mfano, kuna watoto ambao walitolewa shuleni kwa sababu walikuwa wamefunga hijab . Kuna wasichana wa Kiislamu walioenda shuleni na hijab kisha wakatolewa kwa sababu kuna shule ambazo haziruhusu msichana kufunga hijab ama kuwa na nywele za rasta ambazo zinaashiria utamaduni wa Rastafari ambao umelindwa kikatiba. Pia kumekuwa na visa vya utekajinyara na mauji ya watoto. Vile vile, kuna visa vya watoto kujumuishwa kufanya kazi bila kujali kwamba hawajifika umri wa kuajiriwa. Watoto wengine pia wanahujumiwa kimapenzi na kusababishwa kufanya ngono kabla ya muda wao kufika."
}