GET /api/v0.1/hansard/entries/1169307/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1169307,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1169307/?format=api",
    "text_counter": 298,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Tumeangalia zile vipengele tofauti vya sheria hii na tunaona kwamba vyote vitasaidia pakubwa. Ni sheria ambayo italinda watoto wetu katika mambo tofauti. Kwa mfano, katika kifungu cha pili, haki za watoto zimetajwa. Watoto wanastahili kupata maisha na malezi bora, licha ya kuwa wana ulemavu au bila. Tunaona jamii nyingi zikipata mtoto mwenye ulemavu, mara nyingi watoto wale hawapelekwi shule na hawapati huduma za matibabu. Inakuwa ni kama wamelaaniwa. Watoto wote wako sawa na wana haki ya kupata huduma sawa kama watoto. Malezi ya watoto pia yamezingatiwa na mzazi ana jukumu ya kumlea mtoto wake hadi afike miaka kumi na nane. Vile, kama bado yuko shuleni, anahitajika kuendelea kumsomesha hadi ahitimu masomo yake. Tunaona pia katika part 4, kuna mfumo wa usimamizi wa huduma za watoto. Hili ni jambo zuri. Katika kifungu cha tano, inajumuisha huduma katika serikali za kaunti. Kwamba zitahitajika kuwa na makazi ya watoto ambao watakuwa wamepata shida za kisheria au wamekosa mahali pa hifadhi. Watoto wale watapata hifadhi za kuweza kuwaokoa na kuwalinda kutokana na madhara ya umaskini na maovu mengine ya jamiii. Kulikuwa na kisa hapa ambapo baadhi ya watoto waliokuweko katika Mji wa Nakuru waliokuwa wakirandaranda walichukuliwa na kutupwa msituni upande wa Nandi. Jambo hili lilikemewa sana na Bunge la Seneti. Kwa hivyo, sheria hii italinda mambo kama hayo yasiweze kutokea kwa watoto wetu kwa siku za usoni. Pia inatoa mwongozo kwa jukumu la mahakama za watoto kuhusiana na swala hili la watoto. Kuna mahakama maalum za watoto ambazo zinahudumu kuangalia haki za watoto. Kumekuwa na maamuzi tofauti ambayo yametolewa na mahakama hususan kwa watoto ambao ni Waislamu. Wakati wazazi wa mtoto Muislamu wanaachana, mara nyingi kesi zao huudumiwa na Mahakama ya Kadhi. Inasemekana baadhi ya majaji wa Mahakama wameamua kwamba Mahakama ya Kadhi haina uamuzi kuhusiana na maswala ya watoto. Ndoa inapovunjika, maswala ya ni nani ataishi na kusomesha watoto yanaibuka wakati uamuzi ule unafanywa na mahakama ile. Inapofanyika vile, inatakikana koti itoe mwongozo kama watoto wataenda kuishi na mama, wataudumiwa vipi, watasomeshwa vipi na mambo kama hayo. Kwa sasa, wazazi kama hao wanasababika kupata gharama mara mbili. Wanaenda katika Mahakama ya Kadhi iamue kama kuna talaka au hakuna. Baadaye wanaenda katika Mahakama ya Watoto kushughulikia maswala ya watoto, yaani watasomeshwa na kusimamiwa na nani. Hili ni swala ambalo lazima liwekwe wazi kwa sababu wengi wanaona kwamba wakienda katika Mahakama ya Watoto hususan mabibi au wanawake ambao wameolewa, mahakama zile mara nyingi huwa zinatoa maamuzi ambayo inatoa majukumu sawa baina ya mama na baba ya mtoto. Kulingana na sheria ya kiislamu, jukumu ya malezi kama kutoa pesa za matumizi ya watoto na kuwasomesha lamtegemea baba. Kwa hivyo, tofauti hii lazima iangalie kama inawezekana kuwa na nafasi kuwa na marekebisho. Kwa watoto ambao ni Waislamu, Mahakama ya Kadhi itakapokuwa inaamua maswala ya ndoa, iamue pia na maswala ya nani atayekaa na watoto kulingana na sheria ya kiislamu."
}