GET /api/v0.1/hansard/entries/1169645/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1169645,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1169645/?format=api",
"text_counter": 274,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, ningependa kukubaliana na Sen. Olekina kwamba swala lolote ambalo litaadhiri uchumi, mazingara ama binadamu katika jumuiya ya Afrika Mashariki ni swala ambalo linaadhiri nchi zote za Afrika Mashariki. Tunaomba Rais wetu aingilie swala hili na aangalie yale mambo ambayo yanafanyika Loliondo. Hivi karibuni, Loliondo ilisifika kwa dawa ya Babu aliyekua kasisi na alikua akitibu watu na chai yake aliyokua akichemsha. Watu wengi walikua wakienda Loliondo kwa swala hili. Sasa tunaambiwa ya kwamba Loliondo kumeingia maswala ya kuhamishwa kwa Wamaasai. Tunajua Wamaasai wako Kenya na Tanzania. Nafikiri wako pia Uganda. Ni jamii moja hatuwezi kuifungia macho wakati inapata shida. Bi. Spika wa Muda, nasihi Maseneta wenzangu tupitishe Mswada huu kwa sababu utaipa Serikali nafasi ya kujipanga. Tunajua tuna uchaguzi mnamo tarehe tisa mwezi wa nane na Serikali inayoondoka haiwezi kuachia Serikali ingine jukumu ambalo litakua nzito kwao. Tunajua kwamba bajeti ishapitishwa na iliyobakia ni Serikali ni kujizatiti kuhakikisha kwamba bajeti ile inatekelezwa kikamilifu. Tunajua kati ya sasa na mwezi wa nane, kutakuwa hakuna Bunge. Bunge la Kitaifa tayari limeairishwa kwa mara ya mwisho ili kwenda katika uchaguzi. Pia Bunge la Seneti litahairishwa Alhamisi hii. Kati ya sasa na mwezi wa nane, tarehe tisa, kabla ya Bunge jipya kuchaguliwa kutakuwa hakuna Bunge na itakua ni hatari kuacha swala hili likiwa bado halijatatuliwa. Bi. Spika wa Muda, hapo awali kulikuwa na Mswada mwingine ambao ulichapishwa kwa mjadala ambapo walitaka kuongeza hii kiwango kifikie asilimia sitini na tano ya GDP yetu. Tulipojadiliana, tuliona tayari wako katika asilimia sitini na nne nukta tisa. Kwa hivyo, ikiwa wataongeza iwe sitini na tano itamaanisha ile Serikali ambayo itaingia itakua ni pointi moja ya nukta itakuwa imebakia ili kujaza pengo hilo. Tukiangalia hivi sasa, deni la Serikali liko katika Kshs8.7 trillion kufikia mwisho wa mwezi huu wa sita. Iwapo tungekubaliana ni lile swala la maongezeko yao ya awali ina maana kungekukuwa hakuna ongezeko lolote ambalo tumeongeza katika kiwango cha juu cha deni. Tumeona hili ongezeko litaipa Serikali pumzi ili kusaidia kudhibiti uchumi kwa sasa kitambo Serikali ijipange na mambo mengine. Bi. Spika wa Muda, tumeona ipo nia kuweza kuhakikisha deni linadhibitiwa. Bi. Spika wa Muda, tumeona tayari miradi imeanza kufanyika chini ya sheria za Public-Private Partnerships (PPPs) ambayo tulipitisha hapa. Mradi wa Nairobi Expressway tayari umekamilika na sasa unatumika. Miradi mingine kama hiyo pia itaanzishwa. Kwa mfano, barabara ya kutoka Westlands kwenda mpaka Mau Summit. Kwa hivyo, pesa ambazo zingetumika katika miradi kama hiyo, sasa itakuwa inatoka kwa wafadhili moja kwa moja. Wafadhili nao watapata fursa ya kusimamia hiyo"
}