GET /api/v0.1/hansard/entries/1169647/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1169647,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1169647/?format=api",
"text_counter": 276,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "miradi mpaka wajilipe deni zao. Ya Serikali itakuwa tu kuhakikisha zile pesa zinatumika vizuri na pia kudhibiti pesa ambazo mwekezaji atajilipa. Serikali sasa haitakuwa na mamlaka ya kutoa huduma kwa barabara kubwa kama hizo. Hili litakuwa jukumu la wawekezaji. Mpango huu utasaidia pakubwa kuufufua uchumi wetu. Hatimaye, pesa ambazo zingewekezwa katika miradi kama hii, zitawekezwa katika sekta mbalimbali za huduma kwa wananchi, ili tupate maendeleo haraka. Bi. Spika wa Muda, kejeli zimetolewa hapa kwamba Serikali ya “handshake” ndio imesababisha mambo haya. Mambo haya yalikuwepo kutoka awamu ya kwanza ya Serikali hii iliyoko. Baada ya Rais Kenyatta na Mhesh. Raila Odinga kuja pamoja, ndio maswala, ikiwamo uchumi, yakadhibitiwa. Vita dhidi ya ufisadi vikapamba moto. Wengi wanaolalamika kwa sasa wanalalamika kwa sababu wameona kwamba ile mifereji yao ya kupora pesa ya Serikali imefungwa. Bi Spika wa Muda, nikimalizia, naomba uhairishe kupiga kura kwa swala hili mpaka kesho. Hii ni kulingana na Kifungu cha 61(3) cha Kanuni za Bunge la Seneti."
}