GET /api/v0.1/hansard/entries/1170291/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1170291,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1170291/?format=api",
"text_counter": 97,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Tukio hilo liliwatuma kufanya maandamano, wakidhania kwamba watapata msaada. Cha kusikitisha ni kwamba watu watano ambao hawakua katika yale maandamano, walipigwa risasi na kuuawa. Watu hao walikua tu wakiangalia ile vurumai ikitendeka. Ukijumuisha, unapata kwamba zaidi ya watu 13 wameuawa. Bw. Spika, Kuna wimbo nakumbuka ukiimbwa na sasa wananchi wa pale Kajiado wanashindwa; tukimbilie polisi, hapana; tukimbilie msituni mahali ndovu waliko, hapana. Popote watakapoenda watauwawa. Ata pengine wanaona ndovu ni wazuri kushinda askari kwa sababu ndovu waliwauwa watu wanne ilhali askari wamewauwa watu watano na wengine tano wako hospitali. Mkuu wa polisi pamoja na Waziri Matiangi walishughulikie jambo hili kwa dharura kwa sababu vile watu wanavyotaka ni haki yao. Hao majamaa wanaoshughulikia mbuga zetu washughulikie hao wanyama kwa sababu hawa Wanyama wakivamia mashamba ya watu pale Masimba au Laikipia, sio hoja. Ndovu wakiwaua watu sio hoja lakini ingekuwa ni mtu wa Masimba, Rumuruti au Kimanjo huko Laikipia amemuua ndovu mmoja, hapo ndipo ungejuwa ya kwamba Serikali ina mkono mrefu. Je, wanyama wanafaida zaidi kushinda wananchi au wananchi wana faida kushinda wanyama? Hilo ni swali ambalo limekuwa kizungumkuti kwetu na ni jambo la kuvunja moyo sana. Kwa hivyo, Kamati ambayo itapewa jukumu hili washughulikie hili jambo kwa haraka iwezekanavyo ndio watu waweze kupata haki yao. Taarifa hii inasema ya kwamba haijulikani ni nani aliua nani. Hakuna yeyote aliyeshikwa. Hivi majuzi wakati kulisemekana ya kwamba simba alikuwa ameuawa, niliona magari karibu 100 ya askari polisi ikiwa huko ikiwinda wananchi kama swara. Lakini wananchi wakiuawa inasemekana ni kawaida; watu wanapelekwa kwa mortuary na hiyo inakuwa kawaida. Kamati hii ishughulikie jambo hili kwa dharura na wale watu waweze kupata haki yao. Swali ninalojiuliza ni: Nani atakayefidia hizi familia? Asante Bw. Spika."
}