GET /api/v0.1/hansard/entries/1172375/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1172375,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1172375/?format=api",
"text_counter": 530,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": " Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi kuchangia Ripoti hii ya maelewano baina ya nchi hizi mbili. Mwanzo, ikitajwa mambo ya Kenya Defence Forces, imenigusa sana na nikasema na mimi nichangie. Kusema kweli, sisi watu tunaokaa katika maeneo ya misheni za oparesheni tunajua kazi yao wanayoifanya. KDF wanafanya kazi nzuri sana Lamu, haswa askari jeshi wa maji. Kwa sababu tuna ardhi na maji tunajua mambo wanayopitia na kazi wanayofanya. Maelewano haya baina ya nchi hizi mbili yamekuwa yako kulingana na Ripoti. Ni vile tu tunataka yaendelee kuweko. Yale mazuri yalikuwa yakipatikana yazidi kupatikana. Jeshi letu likiwa na maelewano haya ya hizi nchi mbili, zitapata utaalamu mzuri ambao utatusaidia sisi kwa sababu watapata mbinu nzuri za kuweza kutulinda zaidi. Tatizo saa zingine ni kuwako wahalifu. Wapate mbinu za kuweza kuwatoa wahalifu bila kuwadhuru wale ambao si wahalifu. Sisi watu wa Lamu, haswa Kiunga, watu wengi wamekaa na hofu kwa sababu saa zingine wanaogopa ama wanakuwa na hamu. Kwa hivyo wakitumia mbinu walizofundishwa, wataweza kuwatoa wahalifu bila kuwadhuru wananchi na tutakuwa na nchi salama na yenye amani. Ahsante."
}