GET /api/v0.1/hansard/entries/1174373/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1174373,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1174373/?format=api",
    "text_counter": 1118,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "(Likoni, ODM); Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nataka kuafiki Ripoti hii ya Kamati ya kuangalia uwekezaji wa Umma katika utumizi wa fedha za umma. Kamati hii ni muhimu sana, kwa sababu inaangalia takriban mashirika thelathini ya Serikali. Naunga mkono ripoti hii, kwa sababu imeangazia mambo ya kimsingi sana katika utumizi wa fedha za umma, na katika uwekezaji wa mambo ya umma au ile miradi ya umma ambayo inafanyika katika takriban mashirika thelathini. Mwenyekiti amezungumzia sana changamoto ambazo tumezikumba baada ya kupata Ripoti ya Auditor-General, ambayo huwa anaangazia mashirika haya thelathini katika utumizi wao wa pesa wakati wanaweka uwekezaji katika miradi au shughuli muhimu sana za kiserikali. Tunaona kwamba katika mambo ya zabuni, au kwa kiingereza mambo ya procurement, tunaona kwamba mashirika kadhaa yamekuwa hayatumii taratibu za kisheria katika kupeana zabuni. Hivyo basi, wamefanya nchi au Serikali kupoteza pesa nyingi zaidi, na hata pia kuweza kufanya miradi ambayo imewekezwa kuchukua muda mrefu badala ya ule muda ambao ulikuwa umefikiriwa."
}