GET /api/v0.1/hansard/entries/1174381/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1174381,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1174381/?format=api",
    "text_counter": 1126,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Ripoti hii ambayo Mhe. Abdullswamad, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kuwekeza Mali ya Umma amezungumzia leo, iko na mambo mengi sana. Tumeangalia maswala nyeti sana. Kuna suala la Standard Gauge Railway (SGR), ambalo tumezungumzia kwa kina sana. Kandarasi ya SGR inasema kuwa wakati wowote kutakapokuwa na changamoto ama matatizo, suluhu yoyote ikitaka kuzungumziwa, lazima watu wazungumzie kule Beijing. Sasa tunauliza hiyo itakuwa ni bora kwa yule Mchina ambaye tumeingia naye katika mkataba huu, ama itakuwa inatupatia sisi afueni kama taifa la Kenya? Wakati maofisa wa Serikali wanafanya mipango ya uwekezaji wa umma, lazima wafuate taratibu za kisheria. Kila kitu kina taratibu na sheria yake. Lazima tuzingatie kwa hali inayofaa ili tuweze kuhifadhi ama tuwe na value, ama tuwe tutafaidika na zile fedha za Mkenya ambazo anachangia kupitia ushuru. Hili litawezekana kwa kuweza kupata ile miradi, na wakati tunapata miradi tunajua kuwa Mkenya anafaidika kupitia miradi kama hiyo. Lakini ikiwa kutakuwa na utepetevu, iwapo wengine watakuwa wanazembea katika kazi, utapata unaita shirika fulani na unauliza pengine, Je katika maamuzi kama haya, kulikuwa pengine na arafa ambazo zilichangia ya kwamba ile bodi ama wahusika wote waliweza kukubaliana na jambo hilo? Unasema haya tuliyazungumza tu hivi hivi. Ama mtu anasema it was just verbaldiscussion; yalikuwa tu ni maongezi tu ya kiusemi. Sasa unashangaa ya kwamba je maafisa kama hawa ambao wamehitimu na wako katika zile nyadhifa mbazo wamepewa, kweli wanafanya kazi kwa mijubu wa kisheria? Na je, wanafanya kazi ili taifa la Kenya liweze kufaidika na zile fedha ambazo wanaekeza katika hii miradi ya umma, ama mtu yuko pale tu kwa kujinufaisha yeye mwenyewe kibinafsi? Vile vile, pia tunaona wakati ambapo kunapeanwa zile zabuni, unapata ile kampuni ambayo ingepewa ile zabuni haswa kulingana na zile taratibu, unapata inapatiwa hata kampuni nyingine ambayo pengine pia kwa wakati ule wa kuweka maombi ya kupata ile zabuni, hawakuwa wamepeleka maombi kama hayo. Kwa hivyo, tumeona changamoto nyingi sana na tumeona dosari nyingi sana ambazo tumetoa mapendekezo ya kuwa hatua gani ziweze kuchukuliwa. Pia iwapo tutaenda mbele kama taifa la Kenya, tumependekeza mbinu gani watu watakuwa wanatumia kwa mujibu wa kisheria ili uwekezaji wa mali za umma katika taifa letu la Kenya, ziweze kumfaidi Mkenya, na tuseme vile tunasema kwa kiingereza to have value for the money we are using as acountry . Tuweze kusema ya kwamba fedha hizi zimetumika, na zimetumika sawa sawa. Kwa haya mengi ama machache, namuunga mkono Mheshimiwa Abdullswamad katika Ripoti ya Kamati ya PIC. Asante Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda"
}