GET /api/v0.1/hansard/entries/1174421/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1174421,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1174421/?format=api",
"text_counter": 29,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bi. Naibu Spika. Naungana nawe kwa kupeana rambirambi zangu kwa familia, jamii na marafiki wa William Mwamkale Kamoti. Ni huzuni sana kusimama hapa na kuongea juu ya William Kamoti. Alikuwa Mbunge wangu katika Eneo Bunge la Rabai ambalo liko katika Kaunti ya Kilifi. Kamoti alikuwa mwandani wangu. Tulikuwa kama ndugu. Hili ni pigo kubwa sana kwa familia. Kwa niaba yangu, familia yangu ambayo ni moja, jamii yangu na watu wote wa Kilifi, sisi sote tunaomboleza kifo cha Kamoti. Bi. Naibu Spika, kama kila mtu alivyosema, Kamoti alikuwa mtu mungwana. Alikuwa wakili. Wakati mwingine tukipiga kelele na kufanya fujo, alikuwa anatukosoa na kuturekebisha. Alikuwa wakili mwenye maono na alijulikana na kila mtu. Alipenda kufanya urafiki na kuepukana na watu wa fujo."
}