GET /api/v0.1/hansard/entries/1174423/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1174423,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1174423/?format=api",
    "text_counter": 31,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Mheshimiwa Kamoti ameacha familia changa inayohitaji msaada. Familia yake inahitaji kila mmoja wetu kusaidia katika maombi na msaada wa aina yoyote. Alikuwa mmoja wetu katika chama cha ODM ambacho sasa kiko katika Muungano wa Azimio la Kenya. Alikuwa ni sure bet katika kura za tarehe tisa mwezi wa nane ambapo tutampigia ‘Baba’. Alikuwa mmoja wa wagombeaji katika Kaunti ya Kilifi ambapo angepigiwa kura kama Mbunge wa Rabai. Kwa hivi sasa watu wa Eneo Bunge la Rabai ni kama wameshikwa na butwaa na huzuni; hawajui sasa washike mti gani. Lakini tuko na imani ya kwamba yule ambaye ameteuliwa na chama cha Orange Democratic Movement (ODM) ni mdogo wake anayeitwa Mwamkale Kamoti. Tuna imani ya kwamba huyo mdogo wake ana uwezo wa kuingia katika viatu vya ndugu yake japo kuwa ni vikubwa. Sisi tuko na imani kuwa marehemu Kamoti alivyofanya na kuna kwengine alikuwa hajamaliza. Mipangilio kama hiyo inaweza vyema ikiwa ni mtu wa familia anaweza ingia kwenye hivyo viatu an amalize kazi ya ndugu yake aliokuwa akifanya. Mwisho ni kwamba, tunaangalia madereva. Ajali hii ilifanyika kwa sababu dereva wa lori alikuwa anaendesha gari kwa njia ambayo si sawa barabarani. Sasa haitajulikana kwa sababu yeye alienda zake. Hatimaye vile akamuacha Mheshimiwa alipokuwa akikimbia kuingia katika maeneo ya mashimo na dereva kukosa kuweza kuimiliki ile gari. Bi. Naibu Spika, dereva akiwa anaendesha gari usiku ama mchana, ni jambo la muhimu kuzingatia sheria za barabara. Sisi watu wa Kaunti ya Kilifi tumepoteza mshupavu wetu mmoja kama mbunge. Tuna imani ya kwamba katika siku zijazo, ikifika Tarehe Tisa, Mwamkale ataingia katika viatu vya ndugu yake. Tuna imani ya kwamba watu wa Eneo Bunge la Rabai watakuwa na imani na yeye na atafanya kazi pale ndugu yake aliachia na ataweza kuibuka mshindi. Asante Bi. Naibu Spika. Sote tunaomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali palipo wema."
}