GET /api/v0.1/hansard/entries/1174693/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1174693,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1174693/?format=api",
    "text_counter": 28,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante sana Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Nataka kuungana nawe kukaribisha ujumbe kutoka Narok Kaskazini; wakulima wa viazi na shayiri. Ni dhahiri shahiri kwamba ukitembelea sehemu nyingi za Kenya, hasa sehemu ambazo kuna wakulima, unapata barabara sio nzuri. Kwa hivyo, inakuwa vigumu kwao kupeleka mazao yao sokoni. Nimekuwa nikiongea na Sen. Olekina tukiwa naye kwenye Kamati ya Kawi. Alikuwa akiangazia akisema ya kwamba hakuna umeme. Hilo ni jambo ambalo limekuwa kizungumkuti pale. Kwa hivyo, vile ambavyo ningependa kuwaambia, kwa sababu wanawakilisha watu wa kutoka upande huo, ni vizuri waseme ya kwamba Seneta amekuwa akipigania mambo ya umeme iweze kupelekwa sehemu ile, kama vile ndugu yangu alivyosema kuwa amekuwa kipau mbele akipigania mambo ya barabara. Ni vizuri ijulikane ya kwamba Serikali inapaswa kuwa ikiangazia mambo ya barabara. Sio barabara pekee yake, kwa sababu ukipata kitu kama shayiri na vile vile viazi, inakuwa ni vigumu wao kupeleka sokoni. Kama kungekuwa pengine na umeme sehemu zile wangeweza hata kutengeneza"
}