GET /api/v0.1/hansard/entries/1174695/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1174695,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1174695/?format=api",
    "text_counter": 30,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "mahali ambapo wanaweza kuweka viazi vyao na wakati bei imekuwa nzuri wakaviuza. Hilo ndilo jambo linalopaswa kushughulikiwa. Tunampongeza Sen. Olekina leo kwa sababu yeye ni mmoja wa wale ambao wamesema ya kwamba utamaduni mpaka udumishwe. Yeye ni kielelezo tosha katika nchi yetu ya Kenya kwa kuzingatia utamaduni. Si utamaduni peke yake, vile vile, amekuwa akipigania haki za kabila la Wamaasai. Sisemi yeye ni mkabila, lakini anajua mahali ametoka na amekuwa akiwapigania zaidi. Nikimalizia, wakulima watafaidika Zaidi, na tunapaswa kuwainua watu ambao wanaishi maisha ya chini. Wajiunge na serikali ambayo inakuja itakayoongozwa na Mhe. William Samoei arap Ruto, kwa sababu inazingatia watu walio chini kuwainua juu. Wakulima walio chini watainuliwa; wale wote wanaoitwa “ mahustlers ”. Watu wengi Kenya ambao ni “ mahustlers ” wataweza kujimudu kimaisha. Hata wale wote ambao wanavaa nguo za mtumba wa haki kisheria katika nchi yetu ya Kenya kufanya ile biashara yao ndogo ile waweze kuinuliwa. Tukiwainua kiuchumi, itakuwa ni jambo ambalo litasaidia sana. Ninajua hata kama Sen. Olekina ako ule mrengo mwingine, yeye ana imani ya kwamba ‘ hustlers’ mpaka wainuliwe waweze kuwa watu wanaotegemewa katika nchi yetu ya Kenya. Asante sana."
}