GET /api/v0.1/hansard/entries/1174713/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1174713,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1174713/?format=api",
    "text_counter": 48,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Kwanza, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuweza kukuunga mkono kuwakaribisha wanafunzi kutoka maeneo ya Nakuru. Wanafunzi hawa wamekuja kujifunza, kusikia na kujionea kabisa vile mambo ya Seneti yanavyoendelea. Natumaini kuwa baada ya kuona, wataingiwa na moyo ya kwamba siku moja pia wao wana uwezo wa kuja ndani ya Seneti na kuwa Maseneta. Nina hakika kwamba wakitoka hapa leo na kwenda nyumbani, kutakua na Maseneta kadhaa ambao wametengezwa na wataingia hapa miaka mingi ijayo baada ya sisi kuondoka hapa. Bw. Spika, cha pili, nakuunga mkono kwa kuwakaribisha ndugu zetu kutoka pande zile za Narok. Hao ndugu zetu wamekuja kujionea. Hao kama viongozi kutoka huko nyumbani wameweza kujionea vile Seneti inatenda kazi. Ijapokua leo ni siku yetu ya mwisho, wamebahatika kuwa na sisi na wamejionea jinsi kazi inaendelea na vile majadiliano ya Seneti yanatendeka. La muhimu ni kwamba wanatoka eneo la mmoja wetu anayeitwa Sen. Olekina. Yeye ni Seneta wao na ni mchapakazi. Ni Seneta ambaye angefaa kuendelea na kazi, sio kuchaguliwa tena, bali kuendelea. Ndugu zangu kama viongozi, mkirudi nyumbani, muhakikishe ya kwamba Sen. Olekina anarejea hapa Seneti ndio aweze kuwatumikia. Bw. Spika, huyu Seneta ni mchapakazi na sisi tunamjua, na tunawaambia wazi kabisa ya kwamba hamkupiga sipo, bali mlipiga ndipo. Asante, Bw. Spika."
}