GET /api/v0.1/hansard/entries/1174719/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1174719,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1174719/?format=api",
"text_counter": 54,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante Bw. Spika. Ninajiunga na wewe kuwakaribisha wanafunzi katika Kikao hiki cha Seneti. Ningependa kuwaambia kwamba ni muhimu kuweka masomo mbele. Masomo ndio uti wa mgongo wa maendeleo katika nchi yetu ya Kenya. Viongozi wote walio hapa walitilia mkazo masomo wakati walipokuwa vijana. Huu ndio wakati wa kutengeneza maisha yenu ya usoni. Waswahili husema, udongo ufinyange ukiwa mbichi. Mkitia bidii katika masomo yenu, mtapata kile ambacho mnatazamia katika maisha ya mbeleni. Mambo mawili ya kufanya ni kutilia masomo mkazo, kisha kuwa na nidhamu pia."
}