GET /api/v0.1/hansard/entries/1174943/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1174943,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1174943/?format=api",
    "text_counter": 278,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bi. Naibu Spika, tumekuwa na mashindano tofauti tofaufi, kati ya Bunge hili na lile Bunge la Kitaifa, lakini kwa sababu ya umuhimu wa kundi moja kufafanua zile sheria tumeweza kuenda kortini kama Bunge la Seneti na kumekuwa na ushindi katika zile kesi ambazo tuliweza kuzifanya ndani ya muhula huu wa miaka mitano. Ninataka kuwashukuru wale mawakili waliochukua hizo kesi na hatimaye wakalifanya hili Bunge likaweka heshima yake mbele ya Wakenya. Jambo la kusikitisha ni kwamba, ni jambo la Mungu mwenyewe anapenda tulikuwa na mwenda zake Sen. Haji, alikuwa anapenda kuketi mahali pale. Tulikuwa na ndugu yetu Sen. (Dr.) Kabaka, alikuwa anaketi hapa nyuma yangu, tuliwapoteza katika muhula huu. Tulikuwa na ndugu yetu mwingine kutoka Kaunti ya Homa Bay ambaye tulimpoteza mapema baada ya kuingia ndani ya Bunge la 11. Wote hawa tunawaombea Mwenyezi Mungu alaze roho zao palipolala wema. Lingine, kuna mchakato huu wa kuenda kwa kura sasa na tuna hakika na imani ya kwamba katika kura hizi ambazo tutapiga, tunapiga ili tuweze kupewa nafasi tena kule tunakotoka kuridi hapa Seneti. Tuna imani ya kwamba kiongozi wa tano wa Taifa la Kenya atakuwa si mwingine bali ni baba Raila Amolo Odinga. Akiwa yeye yuko hapo, tuna imani ya kwamba nci hii katika uchumi, itaweza kuendelea, maanake ataweza kumaliza mambo ya ufisadi. La mwisho, sisi sote maseneta ambao tunaenda nyumbani, ninataka tujiombee ikiwa mimi ni mmoja wao ninajiombea na ninawaombea wale wote ambao wanaenda kupigania viti tofauti tofauti. Wale wanaotaka ugavana kama ndugu yangu, Sen. Khaniri, yeye akienda kupigania ugavana, mimi nitapiga magoti kwa Mwenyezi Mungu na nitaomba ili aweze kupata nafasi hiyo. Nitamuombea pia ndugu yangu Sen. Mutula Kilonzo Jnr., pia yeye aweze kupata hiyo nafasi ya kuwa gavana wa Kaunti ya Makueni pamoja na wengineo wanaowania hizo nyadhifa zote. Kwa wale ambao wanawania useneta kama mimi, ninawaombea pia. Ninawaweka katika maombi pia hao wapate nafasi ya kurudi hapa Seneti. Akina mama wanaowania viti katika Bunge la Taifa kama Sen. Shiyonga wanawez kupata nafasi. Tunamjua kwa jina la utani. Pole kwa kutumia jina hilo lakini yeye anajulikana sana. Ukisema hivyo, inajulikana ni nani."
}