GET /api/v0.1/hansard/entries/1174987/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1174987,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1174987/?format=api",
"text_counter": 322,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika, kwanza, nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuchaguliwa kama Seneta wa Kaunti ya Mombasa. Pili nashukuru watu wa Mombasa kwa kunipa fursa ya kuwatumikia kwa miaka mitano kama Seneta wao. Furaha niliyo nayo ni kwamba safari yangu ya kuingia Bungeni ilianza mwaka wa 1992. Kabla ya kuchaguliwa, nilikuwa nimejaribu mara nne na Mwenyezi Mungu akanikubalia mwaka wa 2017. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa ni Mkuu. Bw. Spika, nashukuru Ofisi yako, wewe binafsi, pamoja na Ofisi ya Karani wa Seneti. Vile vile nawashukuru Maseneta wenzangu ambao tumehudumu pamoja katika Bunge hili, hususan, wale ambao wamebobea kama vile Sen. Wako, Sen. Orengo, Sen. Khaniri na wengine wote ambao wamekuwa Wabunge kwa muda mrefu. Nilibahatika kuhudumu katika Kamati ya Haki, Maswala ya Kisheria na Haki za Kibinadamu, Kamati ya Uhasibu na Bajeti na Kamati ya Kanuni za Bunge, yani"
}