GET /api/v0.1/hansard/entries/1174989/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1174989,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1174989/?format=api",
    "text_counter": 324,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": ". Katika huduma yetu katika Kamati ya Haki, Maswala ya Kisheria na Haki za Kibinadamu, tuliwahi kuzuru magereza kadhaa nchini Kenya yakiwemo Gereza la Kitui, Nairobi Industrial Area, na magereza ya Kilifi, Kwale na Mombasa. Bw. Spika, nilipata fursa ya kuwatembelea wafungua siku ya ijumaa. Tuliswali pamoja sala ya Ijumaa na wakaniomba kwamba hawana pahali pa kuswali. Nilipeleka swala hii kwa wakuu wa gereza hilo na wakatukubalia kujenga msikiti katika gereza hilo. Tulifungua msikiti huo tarehe ishirini na mbili, mwezi wan ne mwaka huu. Ilikuwa ni sherehe kubwa kwa wafungwa na wale ambao wanahudumu katika gereza hilo. Bw. Spika, nilibahatika pia kuleta maswala ya mauaji ya kiholela ambayo yanafanywa na vitengo vya Serikali, vikiwemo polisi. Ninaashukuru kwamba maombi yangu yalisikizwa kwa makini, na Kamati ikaweza kupitisha ripoti ya kuzuia mauaji ya kiholela. Bw. Spika, nilibahatika mwaka 2020, kuchaguliwa kama Mwenyekiti wa Kamanti ya Kanuni za Bunge yani Committee on Delegated Legislation. Niliweza kuhudumu katika Kamati hilo kwa muda wa miaka miiwili. Tulipitisha kanuni nyingi ambazo zimesaidia kutimiza sheria mbalimbali. Tuliweza kurudisha uhai wa Kamati hiyo na kwa sasa, kila mtu yuko tayari kuhudumu katika hiyo Kamati. Bw. Spika, tulibahatika vilevile kuwa katika ‘ Team Kenya’ ambapo tuliweza kuyazungumzia maswala ya mfumo wa kugawanya fedha za Serikali. Wakati huo, tulipokuwa tunazungumzia swala hilo, Kaunti ya Mombasa ilikuwa inapoteza karibu shilingi billioni moja kila mwaka. Tuliweza kuzuia upotofu huo na kwa sasa, Kaunti ya Mombasa inapokea pesa zaidi kuliko zile walizokuwa wakipokea hapo awali. Bw. Spika, jambo lingine ambalo tuliweza kufanya katika Bunge hili ni uzinduzi wa Kanuni za Kudumu katika lugha ya Kiswahili. Ni matumaini yetu kwamba Bunge lijalo litatoa ripoti zake kwa lugha ya Kiswahili na Sheria nyingi zitaweza kutafsiriwa"
}