GET /api/v0.1/hansard/entries/1174991/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1174991,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1174991/?format=api",
    "text_counter": 326,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "katika lugha ya Kiswahili, ili kuwawezesha Wakenya kufuata mijadala katika Bunge hili na waweze kusoma na kuelewa sheria kwa ufasaha. Bw. Spika, masikitiko yetu ni kwamba tuliweza kupoteza Seneta wanne katika muhula huu, akiwamo Sen. Oluoch kutoka Migori na Sen. Kabaka, ambaye tulikuwa naye katika Chuo Kikuu la Nairobi, kwanzia 1987 hadi tulipomaliza mwaka 1990. Vilevile, kunao Sen. Haji ambaye alikuwa Provincial Commissioner (PC) wakati nilipokuwa shule Mombasa na Sen. Prengei, aliyekuwa wa mwisho kutuwacha. Sen. Kabaka alihudhuria mazishi ya mtoto wangu tarehe 25th, Oktoba, 2018 na vilevile kuapishwa kwa mtoto wangu kama wakili katika Mahakama Kuu ya Kenya, mnamo Juni, 2020, wakati wa Korona. Bw. Spika, ningependa kuwatakia kila la heri wale Seneta ambao wanaaga Bunge la Seneti, kwa nyadhfa mbalimbali, akiwamo Sen. Wako ambaye anastaafu. Wengine wao ni Sen. Orengo, Sen. Khaniri, Sen. Mutula Kilonzo Jnr., Sen. Sakaja, Sen. (Dr.) Ochilo-Ayacko, Sen. (Dr.) Ali, Sen. Kihika, na Sen. (Prof.) Ongeri wanogombea viti mbalimbali za ugavana. Bw. Spika, jambo ambalo linanitia moyo leo ni kwamba, tumeweza kutoa hotuba zetu za mwisho kabla ya Seneta ambaye amehudumu kwa muda mrefu zaidi, Sen. Khaniri. Kwa hivyo, tumepata fursa ya Sen. Khaniri kutuskiza pia. Mara nyingi, alikuwa akiondoka mara nyingi baada ya kutoa mchango wake, kabla ya sisi kuzungumza. Kwa hivyo, tunamshukuru kwamba ametusikiza hivi leo. Bw. Spika, tunakutakia kila la heri kama Spika wetu, unaporudi kuhudumu kama Gavana wa Jimbo la Bungoma. Mwenyezi Mungu akuongoze ili uweze kupata kiti hicho na utakapokuja hapa Bunge, tutakuwa tayari kukusaidia na kukuhudumia kama Spika wetu. Bw. Spika, asante kwa kunipa fursa hii."
}