GET /api/v0.1/hansard/entries/1175218/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1175218,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1175218/?format=api",
    "text_counter": 197,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon Abdullswamad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika. Kwanza, ningependa kuwashukuru watu wa Mvita na Mombasa kwa jumla. Wanamvita walinipigia kura mara ya kwanza na ya pili wakanipigia kura kwa idadi kubwa zaidi. Nashukuru Mwenyezi Mungu kuwa mara ya pili niliporejea katika Bunge hili, Wabunge kwa imani yao wakaamua kunipigia kura niwe Mwenyekiti wa kamati ya Uwekezaji wa Umma kupitia chama cha ODM. Nataka kutoa shukrani kwa party leader wangu Raila Amollo Odinga kwa kuweza kuyaona yale ninayoyafanya. Nilikuwa Mpwani wa kwanza aliyeweza kupatiwa nafasi kugombea na kuchukua kiti cha Mwenyekiti wa kamati ya Uwekezaji wa Umma. Nimeweza kufanya mengi katika Bunge hili. Lakini kuna yale binadamu hukumbukwa nayo. Katika kumbukumbu ya yale niliyoyafanya; kwanza ni kupitisha sheria kuhakikisha nimekataa ubinafsishaji wa Bandari ya Mombasa, kupitisha Miswada na Hoja za kutetea watu wa Mombasa, Mvita na Wapwani kwa ujumla kuhusiana na athari za uchumi wetu kupitia"
}