GET /api/v0.1/hansard/entries/1175242/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1175242,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1175242/?format=api",
"text_counter": 221,
"type": "speech",
"speaker_name": "Laikipia North, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Sara Korere",
"speaker": {
"id": 13134,
"legal_name": "Sara Paulata Korere",
"slug": "sara-paulata-korere"
},
"content": " Mhe. Spika, ninashukuru kwa kunipatia nafasi hii. Kwanza kabisa, napenda kumshukuru Maulana kwa neema na fadhili na kwa kutuhifadhi tangu tulipoanza Muhula huu wa 12 katika Bunge hili. Mhe. Spika, kwa njia ya kipekee nakushukuru wewe kwa kazi nzuri uliyofanya katika Bunge hili. Zaidi ya yote, ningependa kukuarifu kwamba Muhula wa 13 Mwenyezi Mungu akitujalia nitahesabika kama mmoja atakayerudi katika Jumba hili. Mhe. Spika, uko na kazi nzuri na kubwa ambayo umechangia kurudi kwangu hapa. Nawashukuru zaidi wananchi wa Laikipia Kaskazini ambao kwa mara ya kwanza tangu Kenya kupata uhuru walimchagua mwanamke kama Mbunge kutoka eneo bunge hilo ijapokuwa natoka katika jamii ndogo ambayo hata wakati nchi ya Kenya inafanya sensa, sisi tuko katika kundi linaloitwa wengine au kwa Kimombo others kwa sababu sijaona Mdorobo akiorodheshwa katika kuhesabiwa. Mbali na hayo, Mwenyezi Mungu si Mungu wa vitu vya kawaida. Ameweza kunipa kibali na nikaweza kuchaguliwa na walio wengi. Zaidi ya hayo, nimeweza kufanya kazi kwa uadilifu na kwa uaminifu kutumikia wananchi walionituma hapa bila hofu, shaka na kuogopa yeyote yule. Nilipoingia Bunge hili mara ya kwanza, niliteuliwa na chama changu wakati huo na Mhe. Spika nakushukuru maana ni kawaida sana kwamba wale ambao wanapitia uteuzi wa vyama mara nyingi wanadharauliwa na wengine wanafikiria wako hapa kuonekana lakini sio kusikika. Hata hivyo, nashukuru Mwenyezi Mungu leo kwa sababu hata Raisi anayeondoka sasa alipitia kwa njia hiyo hiyo na amekuwa Raisi wa nne wa Kenya. Naamini kwamba hata mimi siku moja nitakuwa Raisi wa nchi hii. Nataka kusema kwamba tumewakilisha watu wetu kwa njia mbalimbali lakini zaidi ya mno kupitia kwa kapu la maendeleo ya maeneobunge (NG-CDF). Kapu hili limesaidia zaidi wananchi wa nchi hii. Ukitazama ugatuzi, gatuzi la NG-CDF ndilo ambalo limeonekana mashinani. Ndilo ambalo limeweza kufanya mengi mashinani na ndilo ambalo limeweza kugusa mwananchi wa kawaida. Inasikitisha sana kwamba ni fedha kidogo sana zinaweza kuwekwa katika kikapu cha NG-CDF. Mimi ninawarai wenzangu ambao watarudi hapa kwamba jambo la kwanza ambalo lazima tushughulikie ni kuinua mapato au ugavi wa NG-CDF. Wananchi wa nchi hii sio sawa. Katika nchi hii, wale ambao tunatoka sehemu zingine tumebaguliwa na The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}