GET /api/v0.1/hansard/entries/1175243/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1175243,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1175243/?format=api",
"text_counter": 222,
"type": "speech",
"speaker_name": "Laikipia North, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Sara Korere",
"speaker": {
"id": 13134,
"legal_name": "Sara Paulata Korere",
"slug": "sara-paulata-korere"
},
"content": "inasikitisha kwamba ndugu aliyeongea, Mhe. Ichung’wah Kimani, ambaye anatoka Kikuyu, walianza kujenga shule huko kabla ya mkoloni kuondoka. Yeye anapewa fedha sawa na mimi ambaye ninaanza kujenga shule. Kwa hivyo, ni matumaini yangu makubwa kwamba jambo hilo litashughulikiwa ili tuweze kuona usawa katika ugavi wa rasilimali katika nchi hii. Nikilamalizia, nataka kusema kwamba wale ambao tuko katika mrengo wa Azimio tunajua Baba the 5th atakuwa Rais. Mhe. Spika, ni aibu kueneza uongo na fitina kwamba Mhe. Raila Amolo Odinga amekashifu sekta ya mitumba. Alisema atafufua ukulima wa pamba."
}