GET /api/v0.1/hansard/entries/1175344/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1175344,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1175344/?format=api",
"text_counter": 323,
"type": "speech",
"speaker_name": "Trans Nzoia CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": "Mhe. Spika, umenisaidia sana. Wakati tuliingia katika Bunge hili, wengine wetu tulikuwa kama councillors wa enzi zile. Hatukujua tunatoka wapi na tunaelekea wapi. Nakushukuru kwa mchango wako kwa kutuelekeza sisi kama Wabunge hadi tukajua ya kwamba tunatoka hapa na tunaelekea kule. Haujakuwa mtu wa kugonganisha watu vichwa katika Bunge hili. Huangalii huyu anatoka kwa kabila gani. Nakushuru sana. Pia, natoa shukrani zangu kwa Rais wa nchi pamoja na Serikali yake yote kwa jumla kwa kazi nzuri ambayo amefanyia hii nchi. Pia, sitasahau Naibu wake. Nikichaguliwa katika Bunge hili, hawa wote walikuwa watu wawili. Pia mimi nilikuwa mwanachama wa Chama cha Jubilee. Saa hizi, mimi ni mgombea huru katika kiti cha akina mama kule Trans Nzoia. Hii ni changamoto ambayo tunaelewa kama wanadamu. Mheshimiwa Spika, haya ni majaribu ambayo tunayaona katika ulimwengu kama bado tuko hai. Nawashukuru wenzangu wote."
}