GET /api/v0.1/hansard/entries/1175364/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1175364,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1175364/?format=api",
    "text_counter": 343,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taita Taveta CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. Hon. (Ms.) Haika Mizighi",
    "speaker": {
        "id": 13274,
        "legal_name": "Lydia Haika Mnene Mizighi",
        "slug": "lydia-haika-mnene-mizighi"
    },
    "content": "Tumekuwa na wakati mzuri na tumekuwa na changamoto hapa Bungeni. Mhe. Spika nakushukuru sana kwa sababu sisi Wajumbe ambao tulichaguliwa kipindi cha kwanza, tunakushukuru sana kwa mwongozo wako. Umetuongoza vizuri, umetupatia mawaidha na umetuongoza kwa hekima ya hali ya juu. Tumejifunza mengi, tumejionea mengi na tumesoma mengi sana ambayo yatatusaidia hapo mbeleni wale wetu ambao tunatazamia kwa kibali cha Mwenyezi Mungu tutarudi hapa katika Bunge la Kumi na Tatu. Naendelea kuwaomba wananchi wa Taita Taveta wanipatie fursa ya kuwatumikia tena kama mwakilishi wa akina mama kwa kipindi cha pili."
}