GET /api/v0.1/hansard/entries/1175669/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1175669,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1175669/?format=api",
    "text_counter": 245,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante Bw. Karani. Nimesimama kulingana na Kanuni ya Kudumu ya 22 ya Seneti, kuhusiana na chama ama muungano wa vyama ambao ndio wengi katika Bunge hili. Swala hili lina umuhimu kwa sababu kura itapigwa na miungano miwili. Kuna muungano wa Kenya Kwanza, na muungano wa Azimio. Ni wazi kwamba, muungano wa Azimio ulikuwa unajumuisha chama kinachojulikana kama United Democratic Movement (UDM). Na hivi sasa, chama cha UDM kimekaa kwa upande wa Kenya Kwanza. Ni chama ambacho katika sheria ya vyama vya kisiasa, kilikuwa katika Muungano wma Azimio na mkataba huo haujafutwa wala kubatilishwa kisheria. Haiwezekani kwamba sheria hii ya vyama ambayo tuliipitisha juzi tu katika Bunge hili, inaweza kudharauliwa, kunajisiwa wakati ambao sisi Maseneta tuliopitisha sheria hiyo tuko hapa. Mpaka sasa, hakujakuwa na talaka baina ya chama cha UDM na muungano wa Azimio. Kwa hivyo, uwepo wao katika muungano wa Kenya Kwanza ni kinyume cha sheria. Sisi kama Bunge la Seneti hatuwezi kukubaliana na swala hilo. Kiongozi wa chama hicho, Sen. Ali Roba yuko hapa na ni Muislamu. Kwa hivyo, anajua kwamba ni haramu kwa mke wa mtu kwenda kwa bwana mwingine bila kupata talaka."
}