GET /api/v0.1/hansard/entries/1175866/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1175866,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1175866/?format=api",
"text_counter": 442,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante Bw . Spika kwa kunipa fursa hii. Kwanza, nachukua fursa hii kukupa kongole kwa kuchaguliwa kama Spika wa Bunge la Seneti. Vile vile, ninachukua fursa hii kumpa kongole Naibu Spika, Mheshimiwa kathuri ambaye pia Bunge lilokwisha tulikuwa tunamwita Kathuri ka mashinani kwa sababu alikuwa anacheza mpira wiga na ni mtanashati sana. Vile vile, ninachukua fursa hii kuwapa kongole maseneta wenzangu wote ambao wamechaguliwa katika Bunge hili la 13. Tuna kazi kubwa ya kufanya, kwa hivyo tungeomba kwamba tushirikiane na tuweze kufanya kazi pamoja ili kupeleka mbele maslahi ya wakenya na wapiga kura wetu kwa jumla. Mheshimiwa Spika umechaguliwa wakati bunge la Seneti kama ulivyozungumza lina vita vya ubabe na Bunge la Kitaifa ambalo linachukua fursa ya ukaribu nafikiri waliokuwa nayo na Serikali iliondoka, kuhakikisha kwamba zile miswada zote ambazo inapitishwa na bunge la Seneti inaendelea kukaliwa. Kuna sheria nyingi ambazo tulipitisha na hazikutumika kwa sababu zilikuwa zinakufa katika lile Bunge la Kitaifa. Kwa hivyo, kwa uzoefu wako na kazi zako nzuri tunahakika kwamba swala hilo halitaweza kutokea katika Bunge hili la 13. Vile vile, Mheshimiwa Spika, nimekusikia ukigusia katika hotuba yako kwamba utahakikisha kwamba maseneta wamewezeshwa kufanya kazi zao za usimamizi. Hiyo ni shida kubwa ambayo tumekuwa nayo. Vile vile, tutawaomba iweze kurekebishwa ili kazi zetu zifanyike. Tunaona kwamba matunda ya ugatuzi yanafikia wananchi katika nchi yetu ya Kenya. Bila ya kusahau, ningependa pia kumpa kongole Mhe. Miraj ambaye ni mtoto wa dadangu na nimefurahi kwamba pia yeye ameweza kuingia katika Bunge la Seneti. Ninamhakikishia kwamba tutaweza kumshika mkono katika Bunge hili pamoja na wale wabunge wote wengine wageni ili tuhakishe kwamba wanatekeleza majukumu yao bila ya matatizo na wanakuwa wenye kusaidia Bunge hili kufikia malengo yake. Asante Mheshimiwa Spika kwa kunipa fursa hii."
}