GET /api/v0.1/hansard/entries/1175868/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1175868,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1175868/?format=api",
"text_counter": 444,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. John Kinyua",
"speaker_title": "The Senator for Laikipia County",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": " Asante sana Bw. Spika . Ninataka kuchukua fursa hii kukupongeza na kumpa heko naibu wako Mhe. Kathuri. Ninawapongeza maseneta wote waliochaguliwa na kushukuru mwenyezi Mungu kwa kutupa fursa hii yakuweza kufika katika Seneti hii. Hasa ninawapongeza watu wa Laikipia kwa kunipigia kura na pia Rais Willliam Samoei arap Ruto. Nasema asante sana. Bw. Spika, nilipokuwa nikipiga kura yangu nilijiuliza maswali matatu. Jambo la kwanza, nilitaka Seneta aliyebobea katika kazi ya gatuzi zetu na ninajua wewe umebobea kabisa. Swali la pili nililojiuliza ni kwamba, ni Seneta ambaye ataelewa mambo ya Serikali Kuu. Nikakumbuka dhahiri shahiri ya kwamba wewe ulikuwa Waziri; nikajua hapo tena umepata ndipo. Swali la tatu ambalo nilijiuliza ni kwamba awe mtu mtenda kazi tena vile ambavyo atachangia katika Kiswahili, kwa sababu mimi napenda kuongea Kiswahili katika Seneti yetu. Nikajiuliza yule Seneta ambaye atafanya Kiswahili kitukuke alafu"
}