GET /api/v0.1/hansard/entries/1175870/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1175870,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1175870/?format=api",
    "text_counter": 446,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. John Kinyua",
    "speaker_title": "The Senator for Laikipia County",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "twende katika upeo wa pili au wajuu zaidi na ukapata ndio. Kwa hivyo, sikuwa na shaka rohoni ya kwamba Spika tuliyenaye amebobea katika kazi yake. Mimi najua ya kwamba tutatoka kikao hiki tukiwa sisi wote tumekubaliana na ninajua ya kwamba sisi sasa tukiwa hapa kama Seneti tutatembea pamoja. Nimemsikia Mhe. Sen. Soipan akisema ya kwamba yeye mwenyewe amekubali ya kwamba hili ndilo jumba kuu ambalo litaendelea kufanya maswala ambayo yanafanywa katika majumba makuu ya jumhuri ya Kenya na hata dunia kwa jumla. Kwa hivyo, nakupongeza na kukutakia mema. Nina kuhakikishia kwamba nitakuunga mkono na naibu wako Mhe. Kathuri ili Seneti hii iendelee kufanya kazi yake. Bw. Spika, umesema ya kwamba utakuwa mbele kuona kwamba kutakuwa na pesa zitakazotumika kufanya uangalizi. Kwa Kizungu inaitwa oversight fund. Utatilia mkazo tuweze kuzipata ili tufanye kazi yetu kwa uadilifu kama tulivyoapa. Mimi nitakuwa mbele kufanya kwa uaminifu na uangalifu na “ewe Mwenyezi Mungu, nisaidie”."
}