GET /api/v0.1/hansard/entries/1175899/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1175899,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1175899/?format=api",
"text_counter": 475,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj Abdillahi",
"speaker_title": "The Nominated Senator",
"speaker": null,
"content": " Shukurani Bw. Spika. Nakushukuru kwa kunipa fursa hii ili niweze kukupongeza kwenye nafasi hii uliyoipata. Nimeinua mkono sana kwa sababu nilitakaa wakenya wasikie sisi wapwani ni watu wa aina gani. Sisi wapwani ni watu wakarimu na Serikali ya William Samoei Ruto pamoja na wajumbe wote waliokupigia kura ya kwamba hii Serikali tuliyoiunda ni serikali ambayo hata wachache wenye tajiriba na uwezo wa kutenda kazi watapata fursa yo kuongoza katika serikali ya William Ruto. Mimi kama mtoto wa mama mboga, ahadi zetu nyingi tulipokuwa katika kampeni zetu tulisema kwamba kura ya mara hii itakuwa kura ya malengo na maono na sio ukabila. Ninawapongeza ndugu zangu kina Sen. Murkomen ambao walikuwa na idadi ya kupigia mtu ambaye angetoka upande wa bara lakini wakatupa sisi wapwani nafasi, kwa sababu ndugu yetu, Mhe. Kingi, una uwezo na tajiriba ya kulipeleka bunge hili mbali. Kongole na ninakukumbusha ya kwamba sisi wapwani ni wastarabu na watu wenye kuweka watu pamoja. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akuongoze na akuwezeshe kuiinua tena sura ya mpwani katika taifa la Kenya. Asanteni."
}